Change Language: English

Kampuni Nambari #1 Kuhodhi Wavuti Tanzania & Wasajili wa .TZ

Vifurushi vyetu vyote vinakuja na anuani za barua pepe bila kikomo, taarifa kuonyesha kama barua pepe zako zimefika mlengwa, uwezo wa kutuma barua pepe kwa watu wengi kwenye kikundi kimoja ulichokusudia na database za MySQL. Anuani zako za barua pepe zinaweza zikafanya kazi kwenye mfumo wa Outlook, BlackBerry, Android, Iphone, Appple Mail pamoja na njia nyingine zinazotumia wavuti.

Furahia huduma kwa mteja saa 24 siku 7 za wiki

Kifurushi cha Binafsi

Jina la tovuti
0.25 GB Nafasi ya Kuhifadhi
0.5 GB Nafasi ya Kuhifadhi
Mkongo wa GB 10 kwa mwezi

Shillingi 115,000 kwa mwaka

Kifurushi cha Ofisi Ndogo

Jina la tovuti
0.5 GB Nafasi ya Kuhifadhi
1 GB Nafasi ya Kuhifadhi
Mkongo wa GB 20 kwa mwezi

Shillingi 185,000 kwa mwaka

Kifurushi cha Kampuni

Jina la tovuti
1 GB Nafasi ya Kuhifadhi
2 GB Nafasi ya Kuhifadhi
Mkongo wa GB 40 kwa mwezi

Shillingi 285,000 kwa mwaka

Kifurushi cha Biashara

Jina la tovuti
2 GB Nafasi ya Kuhifadhi
4 GB Nafasi ya Kuhifadhi
Mkongo wa GB 80 kwa mwezi

Shillingi 385,000 kwa mwaka


Unahamia Extreme Website Technologies?

Basi karibu. Tuna timu mahsusi kwa ajili ya kukusaidia wewe kuhama kutoka msajili mwingine wa tovuti kuja kwetu hata ikiwa ni siku ya Jumapili. Tutakusaidia kuhamisha tovuti yako na tutahakikisha kila kitu kinakwenda vizuri kama inavyotakiwa na tovuti yako kufanya kazi haraka iwezekanavyo. Hii ni huduma isiyokuwa na usumbufu na zaidi, ni bure.

Huduma kwa mteja saa 24 siku 7 za wiki

Tumekuwa tukiwahudumia wateja tangu mwaka 2004 kwa hiyo tunajua vyema kuwa unahitaji msaada wa saa 24 kutoka kwa wataalamu wetu. Timu yetu ya huduma kwa mteja inapatikana kwenye simu kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

Asilimia 99.5 ya ufanyaji kazi wa wavuti

Kila kifurushi chetu cha kuhodhi wavuti kina asilimia 99.5 ya kufanya kazi kwa ufanisi. Tunazichunguza seva zetu kwa kupitia mtoa huduma wa nje ambaye hufanya kazi ya kuangalia utendaji wa kazi wa seva zetu siku nzima. Wafanyakazi wetu wa huduma kwa mteja wanataarifiwa hatua muhimu za kufuata kuweza rekebisha haraka iwezekanavyo.

Njia ya malipo na kuanza matumizi

Inachukua saa moja tu kwa timu yetu kukamilisha malipo ya usajili wa wavuti ikiwa ni katika saa za kazi na itachukua saa 4 hadi saa 24 kabla ya tovuti yako kuanza kazi. Tunapokea malipo kupitia njia hizi:

  • Malipo ya fedha ama cheki ofisini kwetu
  • Malipo ya mtandao wa simu kama Mpesa, Tigo Pesa na Airtel Money
  • Malipo kupitia benki
  • Malipo ya mtandaoni kama Paypal na Kadi za Benki
Tunasherehekea miaka 10 ya kutoa huduma bora ya usajili wa wavuti nchini tangu mwaka 2004 ukisaidiwa na kitengo chetu rafiki cha huduma kwa mteja na chenye kutoa msaada saa 24, siku 7 za wiki.
Extreme Web Technologies ni kampuni nambari moja iliyodhibitishwa na bodi ya usajili wa makampuni ya kuhodhi wavuti Tanzania, tzNIC.

Miundombinu

Kampuni yetu hupewa huduma ya data kutoka kampuni mbili za Kimarekani; Equinix (www.equinix.com) na SARA Computing (www.sara.nl ). Kampuni hizi mbili ndio bora zaidi kwenye soko la uuzaji wa nafasi za wavuti. Vitovu vyetu vya data vimeundwa na kuendeshwa katika mfumo ambao utamridhisha kila aina ya mteja.

  • Uwezo wa kufanya kazi hata pale umeme unapokatika kwa muda mrefu
  • Milango inayofunguliwa kwa sauti ama dole gumba
  • Walinzi saa 24 siku 7 za wiki
  • Makabati
  • Kamera za ulinzi za kurekodi matukio

Njia rahisi ya kuweka web applications

Je unataka kuanzisha blogu yako ama kikundi? Unaweza kufanya hivyo haraka na kwa urahisi kupitia Softaculous inayopatikana kwenye akaunti ya kifurushi yako. Softaculous ni mkusanyiko ya web applications amri zaidi ya 300.