Nini maana ya jina la tovuti?
Kwa lugha nyepesi sana, jina la wavuti ni anuani ya tovuti kwenye mtandao. Kama ambavyo nyumba yako ina anuani yake ya posta ya kipekee basi ndivyo kwa kila tovuti iliyowahi kutengenezwa.
Mfumo wa ugawaji majina wa wavuti ulitengenezwa kwa manufaa ya binadamu. Anuani ya IP inayotumika kwenye mitandao ipo katika mfumo wa tarakimu na inatambulika kama IP kwa kirefu Internet Protocol. Anuani ya IP inaundwa na tarakimu nne zinazotenganishwa na nukta. Mfano wa anuani ya IP ni kama 215.55.258.145. Nafikiri umejionea mwenyewe jinsi gani inavyokuwa ni ngumu kukumbuka anuani hiyo.
Kwa nini ninahitaji jina la tovuti?
Utakapokuwa na jina la tovuti huo utakuwa ni mwanzo wa kutangaza jina lako la biashara kwenye mtandao. Unaweza kusajili jina la biasharayako.co.tz na utaweza kufanya yafuatayo kwa malipo kiduchu.
- Anuani za barua pepe zenye majina binafsi na tofauti na wengine ([email protected])
- Kutumia kwenye tovuti, blogu, duka la mtandaoni na zaidi.
Kodi
Unaweza ukasajili, kulipia upya, kuhamisha na kuendesha kodi mbalimbali za majina ya wavuti kupitia sisi au kwa kutumia kidhibiti kazi cha mtandaoni.
- .co.tz
- .or.tz
- .go.tz
- .ac.tz
- .ne.tz
- .sc.tz .
- hotel.tz
- .info.tz
- .me.tz
- .tv.tz
- .com
- .net
- .org
- .info
- .biz
- .us
- .de
- .es
- .tv
- .mobi
- .co.ug
- .guide
Angalia bei na kama inapatikana
Majina mengi ya wavuti tunazosajili yakiwemo yale ya .TZ yanaanzia bei ya 25,000 kwa mwaka. Bofya kitufe hapo chini ya ukurasa huu kuangalia kama jina unalotaka linapatikana.