Change Language: English

Historia Yetu

2004

Extreme Web Technologies ilianzishwa rasmi na Akberali Sumar aliyekuwa na umri wa miaka 20 pamoja na Mohsin Sumar aliyekuwa na miaka 17. Hawa ni kaka wawili waliokuwa na ndoto ya kuwa na kampuni namba 1 kwenye masuala ya uhodhi wa wavuti nchini Tanzania. Walielewa umuhimu wa kutoa huduma bora na za kipekee kwenye masuala ya wavuti ikiwemo usajili wa majina ya wavuti pamoja na huduma za kuhodhi wavuti ili kuziunganisha na dunia biashara zinazomilikiwa na Watanzania. Ukiacha huduma za wavuti, Akberali na Mohsin walivutiwa sana na kufikiria mbali kuhusu usanifu wa wavuti, utengenezaji tovutina biashara ya mtandao.

2005

Extreme Web Technologies ilizindua tovuti ya biashara pamoja na chombo cha kutafuta vitu yaani search engine waliyoiita Search Tanzania. Search Tanzania ilikuwa moja ya kampuni za mwanzo kabisa za biashara ya mtandao kufanywa na Extreme Web Technologies

Baadae mwakani Extreme Web Technologies walizindua huduma ya kutuma jumbe fupi kwenye mtandao waliyoita Extreme Web SMS. Huduma hii ilifanywa kama nyongeza kwa wateja wote waliosajili tovuti yao na Extreme Web Technologies na ilikuwa ikitoa taarifa za papo hapo kupitia ujumbe mfupi wa maandishi pale panapokuwa na maswali ama usajili kwenye tovuti husika.

2007

Extreme Web Technologies walihamia kwenye ofisi yao ya kwanza iliyopo jengo la Osman Towers, mkabala na Elia Complex Mtaa wa Zanaki katikati ya jiji la dar es salaam.

Baadae mwaka huo huo, Extreme Web Technologies ilitimiza ndoto ya kuwa kampuni nambari moja ya usajili wa wavuti baada ya kusajili wavuti 160 na hivyo kushikilia asilimia 12 ya mauzo katika sekta ya huduma za wavuti.

2008

Extreme Web Technologies ilianzisha moja ya bidhaa zake muhimu iliyoitwa Extreme Mailing List kama njia mojawapo ya kutoa huduma za biashara ya mtandaoni. Huduma hii hutumiwa na biashara mbalimbali kutangaza huduma zao kwa wateja ili kuwavutia zaidi.

Mwaka huo huo kampuni nyingine ya kuhodhi wavuti, SimbaHost, baada ya kuona haiwezi kuenda sambamba na mahitaji ya kampuni, waliungana na Extreme Web Technologies na sasa wanashirikiana nasi katika utoaji wa huduma bora. Kwa pamoja SimbaHost na Extreme Web Technologies inachangia asilimia 30 ya mauzo kwenye sekta ya usajili wa wavuti.

2009

Wafanyakazi wa Extreme Web Technologies waliongezeka kutoka kampuni ya watu wawili hadi kufikia timu inayoundwa na wasanifu wavuti, watengenezaji wa tovuti, masoko na mauzo, utawala na wafanyakazi wengineo.

2011

Tulitimiza moja ya malengo yetu ya muda mrefu ya kuwahamisha wateja wote wa SimbaHost kuja Extreme Web Technologies ili tuweze kuwa na jina moja la utambulisho wa kampuni.

2013

Baada ya kutafakari juu ya utendaji wa miaka iliyopita, menejimenti ikaona ni vyema kama Extreme Web Technologies itakuwa mahsusi kwa ajili ya usajili wa majina ya wavuti, kuhodhi wavuti, haki za kukodisha wavuti pamoja na mambo mengine yanayofanana na hayo. Huduma zingine zikawa chini ya kampuni dada, Rahisisha Solutions Ltd.

2014

Tulitimiza miaka 10 na bado tunafuata kauli mbiu ya kampuni yetu "Kuwa kampuni namba moja ya usajili wa wavuti na kutoa huduma bora saa 24, siku 7 za wiki kupitia timu yetu ya huduma kwa wateja."

Kumbuka: Takwimu za mtandaoni zinatolewa na http://webhosting.info