Change Language: English

24 Apr 2015

Kwa nini unahitaji kuwa na tovuti

Je bado huna tovuti? Zifuatazo ni sababu za kwa nini uwe na tovuti.

1. Tovuti yako hupatikana mwaka mzima kwa siku 7 za wiki, saa 24.
Endapo utafungua tovuti, itakuwa wazi na itakuwa ikitoa taarifa muhimu kwa wateja wako saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki kwa mwaka mzima. Tovuti hutoa taarifa kuhusu biashara yako hata pale unapokuwa umelala.

Ione tovuti yako kama afisa mauzo asiyelala, anayekesha saa 24 siku 7 za wiki kutoa taarifa muhimu kuhusu biashara yako; nini mnajishughulisha nacho, kazi zako za hivi karibuni, bidhaa zako pamoja na shuhuda za wateja wako. Si hayo peke yake; tovuti hukuwezesha kufanya mauzo pia.

2. Tovuti huwasaidia wateja kukupata kwa urahisi
Kadri siku zinavyokwenda ndio jinsi ambavyo imekuwa rahisi kwa watu kupata taarifa mikononi mwao. Uwepo wa simu za kisasa ambazo zinawawezesha watu kutumia chombo cha kutafutia vitu yaani search engine kutafuta vitu wanavyohitaji pale wanapohitaji.

Kwa wastani inasemekana kuwa katika sekunde moja watu elfu arobaini hufanya maulizo yao kwenye mtandao wa Google (source). Hiyo ni sawa na maulizo bilioni tatu na nusu kwa siku na trilioni 1.2 kwa mwaka!

3. Washindani wako wamekuzidi
Kama washindani wako wana tovuti basi watakuwa wana nafasi nzuri zaidi ya kujitangaza. Na wewe ingia kwenye ushindani kwa kuwa na tovuti yako.

4. Anuani za barua pepe hufanya kampuni yako iaminike zaidi
Tovuti huwa na nafasi za anuani za barua pepe ya biashara yako, kwa mfano [email protected] Matumizi ya barua pepe za kibiashara kama hizi zitafanya kampuni yako iaminike zaidi.

5. Tovuti ni njia rahisi ya kutangaza biashara kuliko njia za kizamani
Je ushawahi kuweka tangazo kwenye magazeti au majarida? Hebu jaribu kulinganisha gharama za kutangaza na kwa haraka sana utatambua kuwa gharama za tovuti ni ndogo ukilinganisha na njia za kizamani za utangazaji. Na hata pale unapotangaza kupitia magazeti pamoja na njia zingine, anuani ya tovuti yako huwashawishi wateja kuangalia tovuti yako.

Je unafikiri unahitaji kuwa na tovuti? Angalia huduma zetu za wavuti. Huduma zetu za wavuti zitakuwezesha kukupa anuani ya tovuti, nafasi ya barua pepe na inakuwezesha kufungua tovuti kwa njia iliyo rafiki na simu yako katika muda mfupi kwa kupitia mifano iliyo tayari ya tovuti zilizosanifiwa.

Changia mawazo yako na sababu zaidi kwenye maoni hapo chini!

Kitini hiki kimeandikwa na Mohsin Sumar (@mohsinsumar) ambaye ni mkurugenzi wa Extreme Web Technologies. Mohsin na wafanyakazi wake wa huduma kwa wateja wanajitahidi kadri wawezavyo kutoa huduma za usajili wa wavuti zilizo bora nchini.


Maoni

comments powered by Disqus

Change Language: English

Tafuta